Corona yakwamisha nyongeza ya mishahara

0
44

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ameshindwa kuongeza mishahara ya watumishi wa umma kama wengi walivyotarajia kutokana na athari za #COVID19, ugonjwa ambao umeathiri ukuaji wa uchumi.

Rais Samia amesema hilo wakati akihutubia wananchi na wafanyakazi waliojitokeza katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kwenye maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Kitaifa.

Ametaja sababu nyingine kuwa ni kusudio lake la kufuta baadhi ya tozo na kodi wanazotozwa wafanyakazi, na kwamba kwa kufanya hivyo mapato ya serikali yatapungua kwa muda, hivyo hatoweza kupandisha mishahara mwaka huu.

Hata hivyo ameahidi kupandisha mishahara ya wafanyakazi mwakani, ambapo mbali na hilo katika mwaka ujao wa fedha amesema serikali itaajiri watumishi 40,000 italipa malimbikizo ya watumishi, itaboresha muundo wa utumishi na kupandisha vyeo watumishi wanaostahili.

Watumishi wa umma hawajapandishiwa mishahara yao kwa mwaka wa sita sasa, wakati sekta binafsi ikiwa ni mwaka wa nane.

Send this to a friend