Corona:RC Makonda awataka wakazi wa Dar waliokimbilia mikoani kurejea

0
46

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amewataka wakazi wa mkoa huo ambao waliondoka na kwenda mikoa mingine kwa ajili ya kukwepa virusi vya corona, kurudi na kuendelea na shughuli zao cha kichumi.

Paul Makonda amesema hilo leo Mei 19, 2020 jijini Dar es Salaam wakati akikagua miradi ya maendeleo, huku akiwataka wa miliki wa biashara mbalimbali kurejea makazini.

“Tufungue biashara zetu tufanye kazi. Natoa wito kwa wananchi wote walioondoka kwenda mikoani kwa ajili ya kusubiri corona ipite warudi. Watatukuta tuna afya njema na tunaendelea kuchapa kazi,” amesema Makonda.

Hata hivyo, amewataka watu wote wanapoendelea na majukumu yao kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kunawa mikono, kukaa umbali wa kutosha kati ya mtu na mtu, na kuepuka misongamano ya watu.

Amesisitiza watu kuendelea kuchapa kazi huku akisema kuwa “Mungu ametupendelea.”

Send this to a friend