COVID19: Maagizo mapya 9 ya wizara kuhusu uendeshaji wa ibada

0
37

Katika mwongozo mpya wa kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona uliotolewa leo na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, umeagiza ibada kufanyika kwa muda usiozidi saa mbili, ili kuepusha watu kuwa katika hatari ya maambukizi.

Agizo hilo limetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi wakati akielezea mwongozo huo unaokusudia kudhibiti maambukizi ya COVID19 bila kuathiri shughuli za kiuchumi.

Mbali na agizo la ibada kuwa chini ya saa mbili, wizara imeelekeza yafuatayo kwenye nyumba za ibada:

i. Ziweke vifaa vya kunawia mikono (maji safi tiririka na sabuni au Vitakasa mikonoSanitizers) na muumini atakaye simamia unawaji kwa wote.

ii. Waumini wavae Barakoa

iii. Waumini wakae umbali unaozidi mita moja kutoka mtu mmoja hadi mwingine pande zote.

iv. Taratibu za kufanya usafi na utakasaji wa viti, meza na maeneo wanapokaa kabla na baada ya ibada ufanyike. Alama katika viti ziwekwe kuonyesha umbali wa mita moja.

v. Wazee, Watoto na wale wote wenye matatizo ya kiafya yanayotambulika (Mfano. Kisukari, Shinikizo la Damu, Kansa n.k), wanashauriwa kujiepusha na ibada zenye mikusanyiko ya Watu wengi na wachukue tahadhari zote muda wote

vi. Kama nyumba ya ibada ni ndogo uanzishwe utaratibu wa kusalia nje/maeneo ya wazi au kuongeza idadi ya vipindi vya ibada na kuruhusu idadi ya watu wachache kuingia ibadani na kuzingatia uvaaji wa Barakoa.

vii. Huduma zinazohusisha kugusana ziepukwe

viii. Kuwepo na ujumbe wa mara kwa mara kwa ajili ya kuwakumbusha waumini kuhusu namna ya kujikinga na UVIKO-19 na namba za kuwasiliana na huduma za afya iwapo atapatikana mgonjwa.

Send this to a friend