CWT yataka kikokotoo kirudi kwa wadau kijadiliwe upya

0
21

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimeitaka serikali kukirudisha kikokotoo kilichopendekezwa kwa wadau ili kijadiliwe kwa kuwa sasa kinawaumiza wafanyakazi pale wanapoenda kustaafu.

Katibu wa Chama cha Walimu Mkoa wa Iringa (CWT), Hamisi Chinahova amesema walimu wamekuwa wakifanya kazi kwa kujitolea na weledi mkubwa kuhakikisha wanawafundisha wanafunzi kwa juhudi kubwa licha ya kukumbana na changamoto nyingi, hivyo serikali inatakiwa kukiangalia upya kikokotoo hicho.

Mchungaji Msigwa awataka vijana wa CHADEMA kuacha matusi mtandaoni

Chinahova ameiomba Serikali kutatua changamoto za walimu zikiwemo kulipwa madeni yao ya muda mrefu, uhaba wa walimu na majengo ya kufundishia pamoja na kutopangiwa benki ya kutumia kupitisha mishahara yao kwa kuwa hiyo ni haki ya msingi na serikali inapaswa kuridhia swala hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mohamed Moyo amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, imeanza kufanya maboresho kwenye sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kutatua baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo walimu pamoja na wastaafu katika sekta hiyo.

Send this to a friend