CWT yataka Polisi kutowaingilia

0
62

Baada ya vuta nikuvute iliyotokea kati ya polisi na wajumbe katika Kikao cha Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Rais wa Chama hicho, Leah Ulaya amevitaka baadhi ya vyombo vya Serikali kuacha kuingilia mambo ya chama hicho na wakiache kisimame chenyewe.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha dharura cha Baraza Kuu la CWT Septemba 25, 2023 mkoani Dodoma Ulaya amesema chama hicho kinapitia misukosuko na changamoto nyingi lakini kimesimama imara kwa sababu viongozi wake wako imara, hivyo ametaka viongozi wa chama hicho ngazi ya mikoa kukataa kuingiliwa na mamlaka zingine.

“Tunataka kusimama sisi wenyewe bila kuingiliwa na vyombo vingine, tusiingiliwe kwani tunafanya mambo yetu bila kuvunja sheria, tumechoka kufanya mikutano chini ya Polisi,” amesema Ulaya.

Polisi Kenya wapewa ruksa ya kuua majambazi wanaowashambulia

Vuta nikuvute hiyo ilianza wakati wajumbe wa Baraza Kuu CWT walipoanza kuingia eneo la kikao katika ofisi za CWT na kukuta Polisi wenye silaha wakiwa wamefunga lango la kuingia, huku wakitaka walioko ndani wabaki huko na walioko wa nje wasiingie ndani kwa kile walichosema kuna maelekezo kutoka uongozi wa juu.

Send this to a friend