Dada wa kazi amnyonga mtoto siku mbili baada ya kuajiriwa

0
40

Mtoto Erickson Kimaro (8) anadaiwa kunyongwa na dada wa kazi (jina halijajulikana) Mei 31, nyumbani kwao Kimara Temboni jijini Dar es salaam.

Tukio hilo linadaiwa kutokea majira yaa saa 11 jioni baada ya mtoto huyo kurudi kutoka shuleni, huku ikiwa ni siku mbili mara baada ya binti huyo kuajiriwa nyumbani hapo.

Mama mzazi wa mtoto huyo, Siriwa Kimaro amesema baada ya binti huyo kufanya tukio hilo alimpigia simu kumwambia kuwa mtoto ana hali mbaya na ndipo alipotoka kazini na kuwahi kurudi nyumbani.

“Nafika tu namkuta mwanangu amelala ubavu mdomo na macho yako wazi uso umejaa na shingoni pamevujia damu, kumshika shingoni kawa wa baridi ila mdomo uko wazi kama alikuwa akitafuta hewa,” anasema mama mzazi wa mtoto huyo.

Ameongeza kuwa baada ya kukimbizwa hospitali ya Mloganzila tayari alikuwa amefariki.

Kwa mujibu wa taarifa zinasema kamera ya usalama ‘CCTV’ iliyokuwa nyumbani hapo ilimuonesha binti huyo akimfanyia ukatili ambapo hakujua kama ipo nyumbani hapo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema wanamshikilia binti huyo kwa ajili ya mahojiano zaidi na kuchunguza taarifa iliyoletwa na wazazi wa marehemu.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend