Dada wa kazi raia wa Uganda atolewa figo Saudi Arabia

0
58

Judith Nakintu (38), raia wa Uganda amethibitika kutolewa figo baada ya kuchukuliwa na kampuni ya  Nile Treasure Gate mnamo mwaka 2019 kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za ndani huko Jeddah nchini Saudi Arabia.

Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imethibitisha hilo baada ya kupewa ripoti ya uchunguzi kutoka Hospitali Kuu ya Taifa ya Mulago. Ripoti hiyo inasema kuwa uchunguzi wa madaktari nchini Uganda umethibitisha kuwa figo yake ya kulia ilitolewa.

Hata hivyo mama mzazi wa Judith anasema kuwa, baada ya kufanya kazi karibu miezi miwili Saudi Arabia, mawasiliano yake na familia yake yalikatika, ndipo alipoanza kufuatilia karibu miezi mitatu, na ndipo akaambiwa mwanae amepata ajali.

“Alitufahamisha kwa simu kwamba alipata ajali. Nilikuwa nataka kufahamu familia yake, nikamuuuliza alipata ajali bila kampuni iliyompeleka kujua? Nikawapigia simu kampuni yake nikawaeleza, wakasema hawana taarifa,” amesema mama Judith.

Baada ya Judith kuwasili nchini Uganda akiwa kwenye kiti cha magurudumu, alichukuliwa na gari ya wagonjwa  na kukimbizwa hospitali kuu ya Mulago, ambapo vipimo vya awali vilioyesha kuwa hana tatizo lolote kisha akaruhusiwa kurudi nyumbani.

Mama wa Judith anaeleza kuwa hakuridhishwa na majibu hayo, hivyo akaamua kumrudisha tena hospitali ya Mulago na kufanyiwa uchunguzi upya, ndipo  madaktari wakabaini kuwa  Judith ametolewa figo moja.

Taarifa zinasema kuwa Polisi nchini Saudi Arabia walitoa ripoti zilizoonesha kuwa Nakintu ambaye amepooza, alipata ajali .  Huku Kampuni ya Nile Treasurer ikipokea taarifa kuwa watoto wawili wa mwajiri wake wamefariki dunia kutokana na ajali hiyo, bahati nzuri Nakintu alinusurika ingawa ameumia sana na kusababisha damu yake kuganda.

Rais wa Migrant Workers Voice inayoshughulikia masuala ya wafanyakazi wahamiaji, Abdallah Kayonde amesema kuwa tayari ameiandikia Kampuni hiyo kulipa fidia ya shilijngi milioni 600 za Uganda kwa kitendo cha kutolewa figo ya muathirika huyo na kuuzwa  kinyume cha sheria.

Send this to a friend