Daktari afukuzwa kwa Kumpeleka mtu Mochwari akiwa Hai

1
43

Raia mmoja mkazi wa jiji la Shanghai Nchini China amepelekwa mochwari kwa bahati mbaya akiwa hai akidhaniwa ni maiti.

Mwili wa mzee huyo uliwekwa katika begi maalum la kuhifadhia maiti na kupelekwa mochwari ambapo mhudumu wa Mochwari aligundua kuwa mtu huyo alikuwa hajafa.

Aidha Serikali ya Shanghai imemnyang’anya Cheti Daktari aliyehusika katika Sakata hilo na kumuweka chini ya uchunguzi, pia Maafisa watatu wa afya pamoja na Mkuu wa idara ya uuguzi wameondolewa katika nafasi zao.

Hata hivyo Serikali ya Shanghai imethibitisha kuwa hali ya mzee huyo tayari imeimarika.

Send this to a friend