Watu nane akiwemo daktari wamekamatwa nchini Pakistan wakijihusisha na mtandao wa uhalifu ambao wakati mwingine wamekuwa wakiiba figo za watu bila ya wao kujua.
Mkuu wa Serikali ya jimbo la Punjab la Pakistan, Mohsin Naqvi, ameeleza kuwa Dkt. Fawad Mukhtar alikuwa akifanya upasuaji wa kuondoa figo nyumbani kwake bila idhini ya wagonjwa na kuziuza figo zao kwa wateja matajiri.
Kulingana na Naqvi, mwanaume mwingine ambaye kwa taaluma ni fundi wa magari amekuwa akimsaidia daktari wakati wa operesheni, pia alisaidia katika kuwakusanya wagonjwa kwa ajili ya upasuaji ambapo takribani wagonjwa 328 walifanyiwa upasuaji na watatu walifariki.
Denmark kushitakiwa kwa kuwafunga wanawake vizazi bila idhini yao
Kulingana na wachunguzi, waliokamatwa waliuza figo kwa wagonjwa wa kigeni kwa dola 120,000 (TZS milioni 300) na kwa wagonjwa wa Pakistani kwa rupia milioni tatu.
Kiongozi huyo amesema awali Dk. Mukhtar alikamatwa mara tano, lakini kila mara aliachiliwa kwa usaidizi wa maafisa wa polisi waliopewa rushwa.