Daktari mmoja kutoka Mombasa nchini Kenya, Dias Jumba Wabwire, amesimamishwa kazi na Baraza la Maafisa wa Kliniki baada ya kudaiwa kumbaka mgonjwa aliyekuwa akipata huduma ya usafishaji damu (dialysis) katika Hospitali ya Pandya Januari 31, 2025.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo, Ibrahim Wako ametangaza kusimamishwa mara moja kwa leseni ya Wabwire wakati uchunguzi ukiendelea, na kwamba wanashirikiana na vyombo vya sheria ili kuchukua hatua za kinidhamu baada ya mchakato wa kisheria kukamilika.
Wakati huohuo, Shirikisho la Wanasheria Wanawake (FIDA) limekemea vikali kitendo hicho, likidai kuwa mwathiriwa alikuwa tayari ameshabakwa na mtuhumiwa huyo hapo awali.
FIDA pia imetoa wito wa kukamatwa kwa watu wengine wanaotuhumiwa kuzuia haki kutendeka.
Hata hivyo, Wabwire amekana mashtaka hayo.