Daktari feki akamatwa Muhimbili akifanya utapeli

0
59

Hospitali ya Taifa Muhimbili imemkamata mkazi wa Mbagala mkoani Dar es Salaam aliyejitambulisha kwa jina la Mussa Mawa akijihusisha na utapeli kwa wananchi wanaopata huduma hospitalini hapo.

Mkuu wa Idara ya Ulinzi wa hospitali hiyo, Alfred Mwaluko amesema kuwa daktari huyo feki amebainika akiwa kwenye harakati za kuwatapeli wananchi wanaouguza ndugu yao aliyelazwa jengo la Mwaisela.

Kijana huyo anayekdiriwa kuwa na miaka 35- 40 amesema ana takribani siku sita akifanya utapeli hospitalini hapo, na kueleza kuwa vazi la kidaktari alilianua wakati likiwa limeanikwa baada ya kufuliwa, na kitambulisho alitengenezewa na kijana aliyekuwa akipita eneo hilo.

Akizungumza ndugu wa mgonjwa ambaye amenusurika kutapeliwa, Sada Ramadhan amesema baada ya kukutana na kijana huyo alimrubuni kutoa pesa haraka ili mgonjwa apewe sindano kwa kuwa hali yake si nzuri, na wakati wakitoka nje ya wodi kwa ajili ya mazungumzo zaidi ndipo kijana huyo aliitwa na walinzi wa hospitali.

Askari wakamatwa kwa kusababisha vifo vya watu wawili

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Aminiel Aligaesha ametoa rai kwa watu wote wanaojihusisha na kutapeli wananchi katika eneo la hospitali kuwa ulinzi umeimarishwa na wakijaribu kufanya hivyo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya usalama.

Send this to a friend