Daktari: Mtu mmoja anatakiwa kufanya ngono mara tatu kwa wiki

0
64

Wanaume wanaopenda kufanya ngono mara kwa mara wanadaiwa kuwa kwenye hatari ya kufariki mapema tofauti na wanaume ambao hawafanyi kitendo hicho mara kwa mara.

Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa afya ya uzazi kutoka Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Dkt. Ummukulthum Omar wakati akitoa mafunzo ya afya ya uzazi kwa wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika eneo la Tunguu, Zanzibar.

Dkt. Omar amebainisha kuwa wanaume wanaopenda kufanya ngono hufariki dunia mapema kwa sababu hutumia nguvu nyingi wanapofanya tendo la hilo, hali inayowasababisha kuishiwa nguvu kwenye miili yao.

Athari 7 unazopata kwa kukaa kwenye kiti kwa muda mrefu

Aidha, amesema kitaalamu mtu mmoja anatakiwa kufanya tendo la ndoa mara tatu ndani ya wiki moja ili kuuweka mwili sawa na kwamba anapofanya zaidi ya inavyoelekezwa hujiweka katika hatari.

“Kufanya tendo la ndoa kila siku kunahatarisha afya ya mwili, hivyo ni vyema wanandoa kufanya kitendo hicho kwa kufuata utaalamu kutoka kwa wataalam wa afya na isiwe mnafanya jambo hilo kwa kukomoana,” ametahadharisha Dkt. Omar

Send this to a friend