Wanaume wameshauriwa kushiriki kuwasaidia wake zao katika mchakato wa kujifungua kwa kuwa uwepo wao unasaidia kupunguza kwa asilimia kubwa maumivu ya uchungu pamoja na vifo.
Akizungumza na Swahili Times, Daktari kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, Dkt. Raphael Ung’eng’e amesema pindi wanapopeana faraja, humsaidia mjamzito kupunguza uchungu na hata akijifungua asilimia kubwa huwa salama.
“Ndo maana sasa hivi ukiangalia hospitali nyingi zinatia mkazo kuwa na mwambata wakati wa kujifungua na walitamani sana mwambata huyu awe mwanaume.
Mwanamke wa miaka 70 ajifungua mapacha
Kumpata mwambata especially mwanaume au mumeo au yule ambaye ndiye baba wa mtoto inasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa asilimia kubwa sana, lakini pia inasaidia kumpunguzia mama kiwango kikubwa cha mateso. Kwahiyo wanaume tusiogope kuwa mwambata kwa wake zetu,” ameeleza.
Mbali na hayo amesema mama mjamzito anapokuwa na mume wake wakati wa kujifungua ni rahisi kwake kueleza changamoto anazopitia lakini pia kunapotokea tatizo huweza kupatiwa msaada wa haraka.