Daktari: Pombe kali chanzo cha kuzaliwa watoto njiti

0
69

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dkt. Hawa Ngasongwa amesema moja ya sababu inayochangia watoto takribani 100 kuzaliwa wakiwa na uzito pungufu (njiti) kila mwezi katika hospitali hiyo ni pamoja na unywaji wa pombe kali.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa jengo la wodi ya watoto njiti lililojengwa na shirika la Solidarmed kwa kushirikiana na hospitali hiyo lililogharimu takribani TZS milioni 75.

Tahadhari yatolewa kwa wanawake wanaoweka tumbaku sehemu za siri

“Kila mwezi katika hospitali hii watoto wanaozaliwa njiti ni 100 hadi 200, hii inasababishwa na mama kutokula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha, magonjwa kama shinikizo la damu na unywaji wa pombe kali,” ameeleza Dkt. Ngasongwa.

Ameongeza kuwa mkoani humo, katika kipindi cha mwaka mzima huzaliwa watoto 7,000 na kwa mwezi watoto 600 hadi 700 ambao kati yao watoto 100 hadi 200 huzaliwa njiti.