Daktari: Talaka chanzo cha ugonjwa wa akili kwa wanawake

0
49

Daktari wa Afya ya Akili katika Hospitali ya Wagonjwa wa Akili Kidingo Chekundu Zanzibar, Khadija Omar amesema wimbi la talaka nchini linapelekea wanawake wengi kupata changamoto ya afya ya akili baada ya ndoa kuvunjika au kupewa talaka.

Akizungumza na waandishi wa habari, amesema wanawake wengi Zanzibar katika ndoa huwategemea wanaume kwa sababu ndio wenye kipato na kulisha familia ikilinganishwa na wanawake, hivyo ndoa inapovunjika au mume kufariki mzigo wa kulea humwangukia mwanamke.

“Ukiachwa au mume kufariki, jukumu lote la malazi ya watoto humwangukia mwanamke hivyo hupelekea kupata msongo wa mawazo na kupata tatizo la afya ya akili,” amesema.

WHO yapendekeza pombe ziongezewe kodi

Ameongeza kuwa “hivi sasa pia tumekuwa na changamoto kubwa ya watoto wenye tatizo la afya ya akili ambao tunawapatia huduma ya matibabu hospitalini hapa, wazazi kutoelewana katika familia humwathiri mtoto kisaikolojia na wakati mwingine kukosa haki zake zinazotakiwa.”

Aidha, amesema kwa wastani hupokea wagonjwa wapya wa afya ya akili 150 katika hospitali hiyo wakiwemo wanawake wajane ambao ndoa zao zimevunjika kwa kupewa talaka au mume kufariki.

Send this to a friend