Dalili 5 zinazoashiria moyo wako una tatizo

0
58

Ugonjwa wa moyo umetajwa kusababisha vifo vya watu wengi, huku ukichangiwa na mitindo mibaya maisha.

Chanzo kikuu cha ugonjwa huu ni pamoja na Shinikizo la Damu (B.P), uvutaji wa sigara, kisukari, kukaa sehemu kwa mda mrefu bila kuushughulisha mwili, ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi, historia ya magonjwa yanayoambatana na moyo katika familia na umri.

Kwa msaada wa Tovuti ya Afya ya Complete Care, hizi ni dalili zinazoashiria tatizo kwenye moyo wako.

Maumivu ya kifua
Ishara ya kawaida ya moyo usio na afya ni kifua au maumivu kwenye moyo. Hii inaweza kutokea kwa njia ya kubana, shinikizo au maumivu, na kwa kawaida hudumu zaidi ya dakika kadhaa. Lakini kumbuka kuwa sio shida zote za moyo huja na maumivu ya kifua.

Ikiwa unaanza kuhisi maumivu yakienea kwenye mkono wako wa kushoto, nyuma au begani, unapaswa kumuona daktari kwa vipimo zaidi.

2. Kukosa pumzi
Upungufu wa pumzi ni ishara inayoashiria tatizo la kiafya ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa moyo  na shida zingine za moyo kama vile ugonjwa wa ateri ya moyo, embolism ya mapafu n.k. Ikiwa unakabiliwa na shida ya kupumua, maumivu ya kifua na udhaifu usiojulikana, unashauriaa kumuona daktari.

3. Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida
Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida yanaweza kuwa ishara mbaya kwa moyo wako. Kwa mfano, ni dalili ya mwanzo inayoashiria kushindwa kwa moyo.

4. Kichefuchefu, kiungulia, tumbo, au maumivu ya mgongo
Ingawa dalili hizi zinaweza kuonekana kuwa hazihusiani kabisa na afya ya moyo, mara nyingi zinaweza kuwa ishara za mapema za ugonjwa wa moyo au mshtuko wa moyo hasa kwa wanawake.

Kuna sababu nyingine nyingi ambazo mtu anaweza kuhisi kichefuchefu, kiungulia, msisimko wa asidi, maumivu ya tumbo au maumivu ya mgongo. Lakini ikiwa mojawapo ya matatizo hayo yanajirudia mara kwa mara ni vyema kumuona daktari.

5. Maumivu ya upande wa kushoto
Haya ni maumivu ambayo hutokea chini ya mkono wako wa kushoto kupitia bega lako la kushoto. Hii ni dalili ya kawaida ya mshtuko wa moyo, kwa sababu mishipa ambayo hupeleka maumivu kutoka kwenye moyo wako na mkono wako wa kushoto huenda kwenye sehemu sawa ya ubongo. Kwa hivyo, wakati mwingine inaweza kukuchanganya, maumivu unayosikia moyoni mwako kuhisi kama ni maumivu kwenye upande wako wa kushoto au mkono.

Tafuta matibabu mara moja ikiwa unapata maumivu upande wako wa kushoto, haswa ikiwa maumivu yanaambatana na dalili zingine ambazo tumejadili hapo juu.

Send this to a friend