DAR: Baba adaiwa kuwaua watoto wake kisa hawafanani nae

0
36

Baba wa watoto watatu mkazi wa Chanika jijini Dar es Salaam, Kareem Chamwande anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wawili kwa kuwawekea sumu kwenye juisi akidai hafanani nao.

Tukio hilo limetokea siku ya Jumapili ya Eid Pili usiku, sababu kubwa ikielezwa kuwa baba wa watoto hao alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa mtoto mmoja ambaye ni mdogo wa mwisho si wake na ndipo mke wake alipoamua kuondoka na watoto wake kurudi nyumbani kwao.

Taarifa inaeleza kuwa ilipofika Sikukuu ya Eid Pili, Chamwande alikwenda kuwachukua watoto ili awatoe kwa ajili ya kula sikuku na ndipo alipokwenda kuwapa juisi inayodaiwa kuwa na sumu.

Mtoto mmoja alifariki dunia kabla lengo lake la kujiua halijatimia na ndipo alipompeleka kwa bibi yao kisha kubomoa karo, lengo likiwa bado halijafahamika mara moja ikiwa alitaka kujitumbukiza humo au kumtumbukiza mtoto.

Kijana aiba nguo za ndani za wanawake ili kumzawadia mpenzi wake

Raia wema kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi walifanikiwa kumkamata huku watoto wengine wakikutwa kwenye hali mbaya na ndipo walipokimbizwa hospitalini lakini mmoja alifariki wakiwa njiani.

“Tunamshikilia Kareem Chamwande ambaye anadaiwa kaua watoto wake wawili kwa kuwapa juisi yenye sumu na sasa tunashirikiana na mamlaka zetu za kisayansi kukamilisha uchunguzi huo kwa ajili ya kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa,” amethibitisha Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro.

Send this to a friend