Dar es Salaam hupoteza trilioni 1.4 kutokana na foleni

0
14

Kamishna wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), David Kafulila, amesema kwa wastani jiji la Dar es Salaam linapoteza takribani TZS trilioni 1.4 kwa mwaka kutokana na msongamano wa magari barabarani.

Akizungumza hapo jana wakati akiwakaribisha wawekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya uchukuzi, amesema hali hiyo inachangiwa na wingi wa watu katika mkoa huo.

“Wingi wa watu katika jiji la Dar es Salaam unazidi eneo, watu ni wengi kuliko eneo. Sehemu ya kutumia dakika 10, unatumia dakika 50 kufika,” amesema.

Tanzania imevuka wastani wa unywaji pombe Afrika

Aidha, amesema Serikali inaangalia namna ya kualika wawekezaji katika reli ya Dar es Salaam itakayosaidia katika usafirishaji na hivyo kupunguza foleni katika jiji hilo.

Send this to a friend