Dar es Salaam ya 85 kati ya majiji tajiri zaidi duniani

0
57

Ripoti ya shirika la New World Wealth and Henley Partners imelitaja jiji la Dar es Salaam kuwa jiji la 85 kwa utajiri zaidi duniani na la 12 Afrika inayokua kwa kasi zaidi.

Ripoti ya miji tajiri zaidi duniani mwaka 2023 imeonesha Dar es Salaam ina watu 1,400 matajiri na wenye thamani ya angalau $1 milioni [TZS bilioni 2.3], mamilionea 4 wenye utajiri wa zaidi ya dola milioni 100 [TZS bilioni 234.6] na mtu mmoja ambaye ni bilionea wa dola [zaidi ya TZS trilioni 1.3].

Orodha ya nchi 10 za Afrika zenye mamilionea wa dola wengi zaidi

Barani Afrika, Dar es Salaam ilianguka kutoka 10 bora na sasa iko nafasi ya 12 nyuma ya miji mingine kama Luanda, Accra, Pretoria, Cape Town, Casablanca, Nairobi, Cairo, Johannesburg, Durban, Cape Winelands, na Garden Route.

Afrika Kusini na Misri zilikuwa na miji mingi zaidi barani Afrika katika orodha hiyo, inayoongozwa na Johannesburg ambayo ina mamilionea wa dola 14,600, mji mkuu wa Misri Cairo, 7,800 kisha Cape Town, yenye mamilionea 7,200.

Send this to a friend