DAR: Machinga wapewa siku 7 kuondoa biashara barabarani

0
61

Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ametoa muda wa siku saba wafanyabiashara ndogo wanaofanya biashara kwenye njia za waembea kwa miguu kuondoka.

Makalla ametoa agizo hayo leo Septemba 9, 2021 alipofika katika Soko la Kariakoo kwa ajili ya kusikiliza malalamiko kati ya wafanyabiashara wa maduka na wamachinga katika eneo la Msimbazi.

Mbali na hilo, amewataka wakuu wa ilaya kuratibu maeneo mapya ambayo wafanyabiashara hao watayatumia pindi watakapotoka barabarani, na pia wakutane na viongozi wa wamachinga.

Makalla amesisitiza kuwa machinga kutumia sehemu za waenda kwa miguu kufanya biashara kumechangia uvunjifu wa amani pamoja na ajali kwa kuwalazimisha wanenda kwa miguu kupita sehemu za magari.

Send this to a friend