Dar: Wafanyabiashara waliojenga vibanda katikati ya jiji watakiwa kuviondoa

0
50

Halamshauri ya Jiji la Dar es salaam imewataka wafanyabiashara waliojenga vibanda katikati ya jiji kuviondoa.

Hayo yamejiri leo jijini Dar es salaam katika kikao cha baraza la madiwani wa jiji La Dar es salaam ambacho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza, Mstahiki Meya wa Jiji, Omary Kumbilamoto.

Akizungumza katika kikao hicho Afisa uhusiano wa jiji la Dar es Salaam, Tabu Shaibu ametolea ufafanuzi suala la wafanyabiashara ambapo amesema hawajazuia wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao, bali wanachotakiwa kufanya ni kutojenga vibanda na kuwataka wauze bidhaa zao kwenye meza ili wakimaliza iwe rahisi kuziondoa na kuacha maeneo wazi.

Aidha, amesema mji ni lazima upangike kwa kila eneo linatakiwa kuwa na matumizi sahihi kwani sheria ya mipango miji hairuhusu kujenga vibanda, hivyo amewataka wafanyabiashara hao kutii agizo hilo.

Send this to a friend