Dar yaongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa Red Eyes

0
13

Wizara ya Afya imewaasa wananchi kuacha tabia ya kutumia dawa za macho zisizo rasmi kwa lengo la kutibu ugonjwa wa macho mekundu ‘Red Eyes’ kwa kuwa matumizi hayo yanaweza kupelekea upofu usiotibika.

Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya, Prof. Paschal Ruggajo alipokua anaongea na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar Es Salaam.

“Ugonjwa wa ‘Red Eyes’ hauleti upofu lakini matumizi ya dawa zisizo rasmi na zinazonunuliwa kiholela yanaweza kupelekea upofu usiotibika kama ambavyo inaweza kuwapata baadhi ya wagonjwa waliopata vidonda kwenye kioo cha jicho baada ya kutumia dawa hizo zisizo rasmi,” amesema.

Dkt. Mollel: Serikali inalifanyia kazi suala la sheria kuruhusu utoaji mimba

Amesema, Baadhi ya vitu vinavyotumika ni pamoja na dawa zenye vichocheo vya ‘steroids’ ambazo wananchi wanakwenda kununua wenyewe kwenye maduka ya dawa, tangawizi, chai ya rangi illiyokolea majani, mafuta tete yaliyokuwa yakitumika wakati wa janga la UVIKO – 19, maji ya chumvi na maziwa ya mama, ambavyo vyote vimetajwa kuwa hatari kwa usalama wa macho.

“Mikoa inayoongoza kwa ugonjwa huo ni Dar es Salaam ambapo idadi ya wagonjwa imefikia 6,412, Pwani wagonjwa 4,041, Dodoma 363, Morogoro 307, Mtwara 193, Shinyanga 193, Tanga 190, Lindi 101,” ameeleza.

Ameongeza kuwa mikoa mingine ni Katavi ambao una jumla ya wagonjwa 94, Njombe 81, Ruvuma 77, Arusha 42, Mwanza 40, Mbeya 37, Songwe 33, Rukwa 31, Kilimanjaro 31, Geita 18, Singida 17, Kigoma 13, Simiyu 9, Mara 5 pamoja na Tabora 4.

Send this to a friend