Daraja la Juu la Uhasibu kuanza kutumika Mei 30

0
73

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema Daraja la Chang’ombe lililopo Kurasini jijini Dar es Salaam, litaanza kutumika upande mmoja kupitisha magari Mei 30 mwaka huu.

Ameyasema hayo baada ya kufanya ziara kwenye mradi wa mabasi yaendayo haraka Dar es salaam akianzia barabara ya Kilwa hadi Mbagala.

Waziri amefafanua kuwa, utaratibu utakaotumika, utafuata ratiba maalumu itakayoruhusu Asubuhi wanaotokea Mbagala kutumia barabara ya juu ili kuwawezesha kwenda kwenye shughuli zao, na jioni daraja hilo litatumiwa na wanaotokea mjini kuelekea Mbagala.

Aidha, waziri ametoa shukrani zake kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha fedha za mradi zinalipwa zote na kwa wakati sahihi, na kuongeza kuwa yeye kama Waziri atahakikisha miradi unakamilika kwa wakati likiwemo Daraja la Wami.

Send this to a friend