Daraja la Pangani lafikia asilimia 74

0
73

Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) umesema ujenzi wa Daraja la Pangani (mita 525) na barabara unganishi na mchepuko zenye urefu wa kilomita 25 umefikia asilimia 74.3.

Daraja hilo litaunganisha Mkoa wa Tanga na ushoroba wa Ukanda wa Pwani ya Afrika Mashariki unaoanzia Malindi – Mombasa – Lunga/Horohoro – Tanga – Pangani – Bagamoyo (Makurunge).

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa daraja hilo, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tanga, Mhandisi Msama Msama amesema daraja hilo likikamilika litakuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa usafiri, urahisishaji wa kufanya biashara na kuwezesha wananchi kuchangamana kwa urahisi.