Dawa ya ‘Mkongo’ yapigwa marufuku

0
29

Mwenyeki wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Prof. Hamisi Malebo amesema baraza hilo limeifungia dawa inayoitwa ya Hensha maarufu Mkongo yenye usajili namba TZ17TM0027.

Prof. Malebo amesema dawa hiyo ilikutwa imechanganywa na dawa ya kisasa ya nguvu za kiume inayoitwa Sildenafil kwa jina maarufu la biashara ni Viagra ama Erecto na kusema kuwa baraza litaendelea kufungia wote wanaofanya kazi kinyume na Sheria.

Zimbabwe yaruhusu bangi kuuzwa kwenye maduka

“Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, kuanzia leo tarehe 27 Julai, 2022 limefuta usajili wa dawa ya Hensha alimaarufu Mkongo inayomilikiwa na kituo cha Nyasosi Traditional Clinic, na ihakikishe dawa hiyo inaondolewa sokoni mara moja kuanzia leo vinginevyo hatua kali ya kisheria itachukuliwa dhidi ya Bw. Emmanuel Maduhu,” amesema.

Aidha, Prof. Malebo ameweka wazi kuwa, kwa mganga ambaye anahitaji kutangaza dawa yake ni lazima afuate utaratibu wa kusajili dawa kwa kupima ubora na usalama na baadaye aombe kibali cha matangazo kutoka Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala.