Dawa za kukuzia mifugo zinavyosababisha usugu kwa dawa kwa binadamu

0
63

Wataalam wa mifugo na wafamasia wamesema ukuzaji wa ng’ombe na kuku kwa kutumia antibaotiki unachangia tatizo la usugu kwa asilimia 80 katika kuua vimelea vya magonjwa hasa malaria.

Dawa zilizotajwa kujenga usugu kwa binadamu ni pamoja na chloroquine na Artesunate Plus Sulfadoxine (ASP) zinazotumika kutibu malaria, penicillin na tetracycline.

Wataalam wamesema kutozingatia masharti ya dawa wanazopewa wanyama hao ikiwemo ng’ombe na mbuzi pamoja na zile za kukuza kuku kwa haraka kisha binadamu akala nyama ya mfugo huo, atapata usugu dhidi ya aina husika ya dawa, hivyo kutomtibu pindi akitumia.

Mambo 6 ya kufanya kujikinga na ugonjwa wa figo

Daktari wa mifugo na mtafiti wa magonjwa ya wanyama, Paul Buyugu amesema changamoto zipo kwenye matumizi ya dawa za binadamu na mifugo na shida iliyopo wafugaji wanashindwa kuangalia au kufuata maelekezo ya ukomo wa matumizi.

“Kwa mfano kuna dawa umeandikiwa usitumie nyama siku tano baada ya kumpa mfugo wako, unakuta mfugaji anawapa dawa leo na kesho anauza inaliwa, ndani yake kunakuwa na chembechembe zinazoathiri,” amesema

Ameongeza kuwa “kuna matumizi mabaya ya dawa za mifugo anaambiwa aweke kijiko kimoja kwenye lita tano yeye anakwenda kuweka vijiko viwili kwenye lita mbili, tunaita matumizi mabaya ya dawa, kama ilibidi ikae siku tatu inakwenda kukaa siku nyingi.

Send this to a friend