Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, Jamhuri Wiiliam ameagiza kukamatwa kwa wazazi wa wanafunzi 191 ambao hawajafanya mtihani wa kidato cha pili kutokana na utoro, ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Jamhuri amesema wilaya hiyo itafanya Msako wa nyumba kwa nyumba utakaoenda sambamba na kuwakamata wanafunzi watoro na kuwarudisha shuleni.
“Hili jambo limetushtua, nimeagiza Mkurugenzi, Afisa elimu, watendaji wa vijiji na kata watoto hawa wasakwe popote walipo warudishwe shuleni na isiishie kwao wazazi wao wakamatwe wapelekwe kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine,” ameagiza.
Afisa elimu sekondari wa halmashauri hiyo Patrick Atanas amesema sababu kubwa zinazochangia changamoto hiyo ni pamoja na mimba za utotoni, mwamko mdogo wa wazazi kuhusu elimu, shughuli za migodi, ufugaji na kilimo.
Amteka mtoto wake wa kambo akitaka fedha kutoka kwa mkewe
“Wapo wazazi wanawalazimisha watoto wafeli ili wasiendelee na shule, upande mwingine wanafunzi wanashida wenyewe hawapendi kusoma. Sisi kama idara ya elimu tunachofanya ni kuwaelimisha waone umuhimu wa elimu wawekeze kwenye masomo,” amesema.