DC aagiza Lema akamatwe kwa uchochezi

0
40

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali ameliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta na kumkamata Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema kwa madai ya kutoa kauli za uchochezi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Oktoba 24 mwaka huu.

Katika mkutano huo uliofanyika katika Kata ya Korongwe, jimbo la Nkasi Kaskazini, Godbless Lema akiwa na viongozi pamoja na wafuasi wa chama hicho ameonekana kutamka neno ambalo limetafsiriwa kuwa ni kutaka wanaume wamuue mtendaji Daud Ismail ambaye wananchi wamelalamikia utendaji wake katika mkutano huo.

Hata hivyo, Lema amekanusha madai hayo ya uchochezi, akisema kuwa kauli yake ilikuwa ya kisiasa na haikuwa na nia ya kuleta madhara yoyote kwa Mtendaji huyo.

DC Lijualikali amesisitiza kuwa kauli kama hizo za vitisho hazipaswi kuvumiliwa, na kwamba hatua zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya viongozi wenye ushawishi wanaotoa kauli kama ambazo zinaweza kusababisha taharuki miongoni mwa wananchi na kuleta hatari kwa maisha ya watu.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend