DC aagiza msako wa bodaboda waliotoboa eksozi

0
41

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro ameagiza kufanyika msako mkali wa kuwakamata waendesha pikipiki (bodaboda) waliotoboa eksozi za pikipiki.

Amesema vitendo hivyo vinasababisha kelele na milipuko mikubwa inayohatarisha maisha ya wananchi hususan ni wale wenye matatizo ya presha.

“Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani ninaagiza anzeni mara moja msako wa kuwakamata bodaboda wote waliotoboa eksozi zao. Milipuko hii ya kelele inahatarisha maisha ya wananchi hasa wale wenye presha. Hatuwezi kuvumilia hali hii iendelee,” amesema.

Ameongeza kuwa Serikali ina wajibu wa kulinda usalama na ustawi wa wananchi wake.

Send this to a friend