DCEA: Vijana wa vyuo wanaongoza matumizi ya dawa za kulevya

0
86

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kukevya (DCEA) imesema kundi la vijana wasomi wa vyuo vikuu ndio linaloongoza kwa matumizi makubwa ya dawa za kulevya ikiwemo uchepushwaji wa kemilaki bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini hati ya ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kudhibiti uchepushwaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye athari za kulevya, amesema kundi hilo liko kwenye hatari ya kuharibika kiafya, kushindwa kupata watoto hapo mbeleni na hata kupoteza ajira zao kwa wageni.

“Tumefanya utafiti mdogo na tumegundua vijana wasomi wanaongoza kwa matumizi ya dawa za kulevya, na pia wengine wanasoma nchini Marekani na wengine vyuo vikuu hapa nchini na nchi nyinginezo, tutakosa wataalam wasomi baadaye sababu ya matumizi ya dawa tiba zenye asili ya madawa ya kulevya,” amesema.

Aidha, amewasihi wauzaji kemikali hizo kuwa makini ili kudhibiti matumizi ya dawa hizo hususani kwa vijana.

Chanzo: Habari Leo