DCEA yakamata wamiliki wa kiwanda bubu cha kuzalisha biskuti zenye bangi

0
105

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imewakamata wamiliki wa kiwanda bubu cha kuzalisha biskuti zenye viambata vya dawa za kulevya aina ya bangi na skanka eneo la Sinza, Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo amesema wazalishaji wamekuwa wakiwauzia zaidi wafanyabiashara wa madini ili kuwapa wanaofanya nao biashara hizo kwa lengo la kuwaibia.

“Eneo la Sinza walikamatwa watu wawili wamiliki wa kiwanda bubu kinachotengeneza biskuti zinazochanganywa na bangi kisha kuzisambaza katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Lindi na Mtwara.,” ameeleza.

Send this to a friend