Deni la Kenya kwa Benki ya Dunia lapanda na kufikia TZS trilioni 25

0
34

Deni la Kenya kwa Benki ya Dunia limepanda hadi kufikia Ksh1.5 trilioni [TZS trilioni 24.96] mwezi wa Juni kutokana na ongezeko la mikopo na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Kenya.

Takwimu kutoka Benki Kuu ya Kenya inaonesha kuwa deni hilo lilikuwa Ksh1.57 trilioni (TZS trilioni 26.1] mwishoni mwa mwaka wa fedha uliopita, likiwa limeongezeka kutoka Ksh1.46 trilioni [TZS trilioni 24.3] mwishoni mwa Mei. Ongezeko hilo la Ksh110.9 bilioni [TZS trilioni 1.8] linamaanisha kuwa karibu asilimia 60 ya jumla ya deni la Kenya kwa taasisi za fedha za kimataifa linamilikiwa na Benki ya Dunia.

“Kuongezeka kwa Ksh309.4 bilioni [TZS trilioni 5.1] katika mikopo ya nje kunaweza kuelezewa kwa utoaji wa fedha uliofanywa mwezi huo na kupungua kwa thamani ya sarafu ya Kenya,” ilisema hazina katika taarifa.

Watanzania wawili wapotea Israel, Serikali yaendelea kuwatafuta

Kwa mujibu wa takwimu, asilimia 73 ya deni la nje la Kenya linadaiwa na Benki ya Dunia, Eurobonds, China na Benki ya Maendeleo ya Afrika na kufikia jumla ya Ksh3.97 trilioni [TZS trilioni 65.9].

Hazina inakadiria kuwa, gharama kwa ajili ya deni kwa mwaka wa fedha wa sasa zitapanda hadi Ksh1.62 trilioni [TZS trilioni 26.9] na asilimia 38 ya gharama hizo zitakwenda kwa wakopeshaji wa nje, kiasi hiki cha Ksh1.6 trilioni kitakachotumika kwa huduma ya deni kinawakilisha asilimia 64 ya mapato ya kawaida ya jumla ambayo Hazina inatarajia kukusanya katika mwaka unaokamilika Juni 2024.

Send this to a friend