Deni la Taifa laongezeka kwa asilimia 7.6

0
42

Deni la Taifa (Tanzania) limefikia TZS trilioni 59 hadi kufikia Disemba 2020 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 7.6 ikilinganishwa na TZS trilioni 54.8 kwa kipindi kama hicho mwaka 2019.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Sillo Baran, alipokuwa akiwasilisha taarifa kuhusu tathimini ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2016/2017 mpaka 2020/2021.

Baran ambaye pia ni Mbunge wa Babati Vijijini amesema kuwa kati ya kiasi hicho deni la ndani limefikia TZS trilioni 16.2 na deni la nje TZS Trilioni 42.8.

Ameeleza kuwa kuongezeka kwa deni la taifa kumetokana na ukopaji kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aidha, licha ya deni hilo ni himilivu kwa vigezo vyote vya kimataifa, serikali imeshauriwa ione haja ya kujipima uhimilivu wakekwa kutumia kiashiria cha makusanyo ya mapato ya ndani kwa pato la Taifa.

Send this to a friend