Denmark kushitakiwa kwa kuwafunga wanawake vizazi bila ridhaa yao

0
28

Makumi ya wanawake wa Greenland wanapanga kuishtaka Serikali ya Denmark kwa kile walichodai waliwekewa koili ya kuzuia mimba bila idhini yao katika miaka ya 1960.

Kikundi hicho chenye wanawake 67 ambao baadhi yao walikuwa wadogo kati ya wasichana 4,500, wanadai waliwekewa kifaa cha IUD na madaktari wa Denmark katika kampeni ya kudhibiti idadi ya watu wa Greenland kati ya mwaka 1966 na 1970, pindi nchi hiyo inayojitawala kwa sasa ikiwa chini ya Denmark.

Wanawake hao wameomba fidia kutoka serikalini takribani £35,000 [TZS milioni 105.9] kwa kile wanachosema kitendo killichofanyika ni ukiukaji ambao umekuwa na madhara makubwa katika maisha yao ikiwa ni pamoja na wengi wao kushindwa kubeba mimba, na kama serikali haitatii, wanawake hao wanapanga kupeleka kesi yao mahakamani.

Ufaransa inapambana kudhibiti kunguni kabla ya mashindano ya Olimpiki mwakani

“Mawakili wetu wana uhakika sana kwamba haki zetu za binadamu na sheria zilivunjwa,” mwanasaikolojia na mwanaharakati wa wanawake amesema huku akiongeza kuwa ingawa alipata mtoto, lakini wanawake wengine wengi hawakuweza kushika mimba. “Ilikuwa sawa na kuwafunga wasichana tangu mwanzo.”

Aidha, uchunguzi unatarajiwa kukamilika mwaka 2025, lakini wanawake hao ambao baadhi yao wana umri wa miaka 70, wanataka walipwe fidia yao sasa hivi.

Send this to a friend