Dereva akamatwa kwa tuhuma za kumgonga na kumuua trafiki Mwanza

0
72

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia dereva wa gari la Shule ya Msingi Nyamuge, Philipo Mhina kwa tuhuma za kumgonga na kusababisha kifo cha Askari Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, Sajenti Stella Alphonce.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea leo asubuhi ya eneo la Nyamuhongolo mkoani humo wakati askari huyo alipokuwa akitekeleza majukumu yake ya ukaguzi barabarani.

TCAA yafafanua kuhusu kibali cha Helikopta ya CHADEMA

Kamanda Mutafungwa amesema askari huyo alisimamisha gari hilo kwa ajili ya ukaguzi, baada ya gari kukutwa na kosa na kumtaka dereva arudishe gari nyuma kwa ajili ya usalama, ndipo alimgonga askari huyo kwa nyuma na kusababisha kifo chake.