Dereva aliyetumia gari la serikali kubeba dawa za kulevya asimamishwa kazi

1
20

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk. John Pima amesema halmashauri hiyo imemsimamisha kazi dereva wake, Athuman Magio kwa tuhuma za kutumia gari la halmashauri kusafirisha dawa za kulevya.

Dk. Pima amesema tukio hilo limetokea siku ya sikukuu ya Eid El Fitri, Mei 2 mwaka huu ambapo mtuhumiwa alikamatwa na polisi akisafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi zaidi ya kilo 500 katika wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.

Aidha ameeleza kuwa siku ya tukio dereva huyo alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Landcruiser yenye namba za usajili STJ 7333 wakati alipoagizwa kwenda wilaya ya Karatu kuwachukua maofisa wa Almashauri hiyo waliokuwa wilayani humo kwa shughuli za kikazi.

Taarifa inaeleza kuwa aliporudi Arusha, aliegesha gari hilo kwenye ofisi za Jiji na kulikabidhi kwa walinzi kwa kuliandikisha kwenye kitabu cha walinzi, kisha jioni alirudi kulichukua akiwadanganya walinzi kuwa anaendelea na kazi, na ndipo alikamatwa na polisi akiwa na shehena hizo wilaya ya Rombo.

Send this to a friend