Dereva bodaboda afumaniwa na mke wa Kasisi, auawa na wananchi

0
64

Mwendesha bodaboda mwenye umri wa miaka 38 ameuawa baada ya kukamatwa akiwa na mke wa kasisi katika kijiji cha Kumbatha, eneo la Gwasii Mashariki nchini Kenya.

Marehemu, aliyetambulika kama Wilson Onjiro Otieno, anadaiwa kwenda kwenye nyumba ya kasisi Jumapili usiku ili kukutana na mke wa kasisi bila kutambua kuwa kasisi huyo alikuwa ndani ya nyumba hiyo.

Kulingana na Chifu Andrew Ombisa wa eneo hilo, marehemu anasemekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa kasisi huyo kwa muda mrefu, na kwamba alikuwa akitumia fursa ya kutokuwepo kwa kasisi kipindi alipokuwa nje ya nyumba kwa ajili ya shughuli za kiroho katika Kitongoji cha Sindo.

Mwanaume ajichoma moto baada ya mkewe kukataa kumpikia kuku

Baada ya mabishano ya muda mrefu, marehemu alikwenda nyumbani kwake na kurejea akiwa na silaha ili kumshambulia kiongozi huyo, ambapo Kasisi alipiga filimbi iliyowatahadharisha watu ambao walimvamia na kumuua na kisha mwili wake kutelekezwa katika shule ya msingi ya Kumathi ambako ulipatikana Jumatatu asubuhi.

Hata hivyo, Kasisi huyo, mkewe na watoto wanaripotiwa kutoroka nyumbani baada ya tukio hilo.

Send this to a friend