Dereva Bodaboda arejesha milioni 115 alizookota

0
42

Dereva bodaboda nchini Liberia amezua gumzo baada ya kupata na kurejesha $50,000 (TZS milioni 115) za mfanyabiashara mwanamke zilizopotea katika Jimbo la Nimba, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Emmanuel Tolue aliona fedha hizo zikiwa kwenye mfuko wa plastiki barabarani, na akamsikia mwenye nazo, Musu Yancy akitoa taarifa kwenye redio kuomba atakayaezipata azirejeshe.

Kutokana na kitendo hicho dereva huyo amepewa zawadi ya $1,500 (TZS milioni 3.5).

Mwanadada huyo alifurahi sana kupata fedha hizo, huku pongezi pia zikienda kwa kijana huyo kwa wema alioutenda.

Send this to a friend