Dereva Bodaboda ashikiliwa kwa tuhuma za kumuua Stephen Chalamila

0
38

Jeshi la Polisi mkoani Songwe linamshikilia mwanaume mmoja dereva wa Bodaboda kwa tuhuma za mauaji ya Stephen Evaristo Chalamila (23) mkazi wa Chapwa ‘A’ Wilaya ya Momba mkoani humo.

Tukio hilo lilitokea Novemba 26, mwaka huu, majira ya saa 4:30 usiku ambapo alivamiwa na kushambuliwa na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake amelala baada ya kuvunja mlango na kukatwa na kitu chenye kali kichwani na mikononi na kusababisha kifo chake.

“Hadi sasa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limemkamata mwanaume mmoja bodaboda kwa mahojiano ili kufahamu chanzo cha tukio hilo na wengine waliohusika ni akina nani,” imesema taarifa ya Polisi.

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kufanya matukio ya kiuhalifu kwani halitasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayehusika.

Send this to a friend