Dereva Taxi kizimbani kwa 'kumteka' Mo Dewji

0
45

Dereva Taxi, Mousa Twaleb (46) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Mei 28, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kumteka Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group)  , Mohammed ‘MO’ Dewji.

Twaleb amesomewa mashtaka hayo mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Shtaka jingine linalomkabili mtuhumiwa huyo ni kujipatia fedha kwa kutumia nguvu.

Mfanyabiashara MO Dewji alitekwa na watu wasiojulikana alfajiri ya Oktoba 11, 2018 katika Hoteli ya Colosseum iliyopo jijini Dar es Salaam, na alipatikana siku 9 baadae (Oktoba 20) katika eneo la Gymkhana baada ya kudaiwa kutelekezwa na watekaji hao.

Katika msako wa polisi, jumla ya watu 12 walikamatwa wakihusishwa na tukio hilo.

Send this to a friend