Dereva wa basi aliyesababisha ajali Mwanza ashitakiwa kwa makosa 64

0
45

Dereva wa basi la Asante Rabi, Shedrack Swai (37) aliyesababisha ajali Oktoba 22, 2024 eneo la Ukiligulu, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Misungwi na kusomewa mashtaka.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ramson Salehe ameieleza mahakama kuwa mshtakiwa anashtakiwa kwa makosa 64 ikiwemo kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya watu tisa, kujeruhi 54 na uharibifu wa mali pamoja na miundombinu.

“Mshtakiwa siku ya Oktoba 22,2024, ukiwa dereva wa gari lanye namba za usajiri T. 458 DYD aina ya Yutong basi uliendesha gari hilo kwa uzembe katika barabara ya umma Mwanza-Shinyanga eneo la Kijiji cha Ukiriguru wilayani Misungwi ambapo ulilipita gari lingine bila kuchukua tahadhari na matokeo yake ukaligonga gari lingine lenye namba za usajiri T. 281 EFG aina ya You tong basi na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali,” amesema Salehe.

Baada ya kumsomewa makosa hayo, mshtakiwa alikiri makosa hayo 64 na kurejeshwa rumande baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili.

Send this to a friend