Dereva wa Bolt ajivunia mafanikio yake

0
45

Na Mwandishi Wetu


Fabian Shao (32) anasema kuwa baada ya kuacha kazi ya udereva katika shirika moja la kimataifa na kuamua kujiajiri na kuwa dereva wa Bolt amepata mafanikio makubwa katika maisha yake.


Shao, ambaye ni mkazi wa Chanika Dar es Salaam ana mke na Watoto watatu, anasema kuwa amefanya kazi na shirika hilo ambalo akutaka liandikwe kwa miaka miwili lakini baada ya kuingia bolt amepata mafanikio makubwa pamoja na kuwa mjasiriamali kwa kufungua biashara.


Anaeleza kuwa hakuwa rahisi uamuzi aliochukua wa kuacha kazi pamoja na uamuzi wa kuchukua mkopo wa gari wa riba nafuu kwani mke wake hakuamini kuwa angeweza kufanikiwa.


Shao, anasema kuwa kilichomsukuma kuchukua mkopo ni kutokana na kufanya kazi kwa muda mrefu bila mkataba wa kidumu huku mshahara anaolipwa kutokidhi mahitaji yake na kushindwa kutimiza malengo yake.


Anasema kuwa ilifika wakati, kuwalipia ada Watoto wake ambao mmoja anasoma kidato cha kwanza na wapili darasa la tano na watatu darasa la tatu ilikuwa ngumu, kutokana na kipato kidogo na kukosa chanzo kingine cha mapato.


“Nilikuwa nafanya kazi katika shirika moja kubwa tu hapa Dar es Salaam, kama Dereva, nimefanya kwa Miaka miwili bila kuona nikisogea kimaendeleo ndipo nilipoamua kuacha kazi na kuchukua mkopo na kununua gari kwa ajili ya Bolt,” amesema na kuongeza kuwa;


“Niliweka malengo na nimefanikiwa, ndani ya Mwaka mmoja nimemaliza mkopo, na kwa sasa nimenunua gari nyingine, Watoto wangu wana uhakika wa kusoma, nimefungua sehemu ya kuosha magari (car wash) na nimempa mtaji mke wangu wa kufuga kuku wa kisasa, kwakweli najivunia sana kuwa Dereva wa Bolt,” amesema


Amewapa ushauri vijana kufanya kazi ya usafiri mtandaoni na Bolt kwani ni kampuni ambayo inawasaidia vijana kujikwamua katika maisha pamoja na kutimiza malengo yao.


Ameongeza kuwa utaratibu wa bolt waliouweka wa kuwajali madereva wake kwa kuwapa elimu ndio kitu kilichomvutia kwani wanakipa mwanga wa nini cha kufanya katika kazi yako ya udereva wa bolt.

Send this to a friend