Dereva wa Mkuu wa Mkoa azimia baada ya mwanae kupata ajali na gari ya RC aliyochukua bila ruhusa

0
48

Dereva wa Mkuu wa Mkoa wa Mara amelazwa hospitali baada ya kuanguka kwa presha alipofika eneo ambapo mtoto wake mwenye umri wa miaka 26 alipopatia ajali wakati akiendesha gari ya Mkuu wa Mkoa.

Mtoto huyo aliyechukua gari bila ridhaa ya baba yake, pia amelezwa hospitali kutokana na majeraha aliyopata kufuatia ajali hiyo iliyotokea jana Agosti 4, 2019.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara amesema dereva huyo akipona atachukuliwa hatua kwa uzembe wa kuacha gari hadi ikachukuliwa na mwanae, na kwamba kuna uwezekano huwa anamwachia kila mara anapokwenda nalo nyumbani kwake.

Aidha, ameweka wazi kuwa, mtoto huyo akipona naye atachukuliwa hatua za kisheria.

Kamanda wa Polisi amesema kuwa mtoto huyo alichugua gari hilo baada ya baba yake kuliacha nje likiwa linaunguruma kutokana na kupata mgeni wakati alipokuwa akijiandaa kulirudisha ofisini kwa mkuu wa mkoa alipomaliza kuliosha.

Wakati akiliendesha, alipofika katika eneo la Kwangwa, Musoma gari ilimshinda mtoto huyo kisha ikatoka nje ya barabara na kugonga ukuta wa daraja.

Send this to a friend