Dhahabu ya magendo yenye thamani ya bilioni 3.4 yakamatwa bandari ya Dar es Salaam

0
78

Serikali imekamata kilo 15.78 za dhahabu zenye thamani ya shilingi bilioni 3.4 katika bandari ya Dar es Salaam zilizokuwa zikisafirishwa kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar.

Akizungumza na vyombo vya habari, Waziri wa Madini, Antony Mavunde amesema Watanzania watatu wamekamatwa wakijihusisha na shughuli hiyo, na endapo watapatikana na hatia adhabu kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kufungiwa maisha kujihusisha na sekta ya madini.

Aidha, Waziri Mavunde amewataka Watanzania kutambua mchango mkubwa unaochangiwa na mapato ya sekta ya madini katika kusaidia huduma za kijamii na maendeleo ya taifa.

Sekta ya madini inachangia takriban asilimia tisa ya Pato la Taifa (GDP) la Tanzania, lakini serikali inaamini kuwa mchango huo unaweza kuvuka asilimia 10 mapema kabla ya muda uliopangwa wa mwaka 2025.

Send this to a friend