Diamond afichua kiasi ambacho Zuchu atalipa akisitisha mkataba WCB

0
84

Msanii wa muziki na mmiliki wa lebo ya Wasafi, Diamond Platnumz amefichua kuwa endapo msanii wake Zuchu atasitisha mkataba wake katika lebo hiyo, atalazimika kulipa TZS bilioni 10.

Diamond ameweka wazi hilo alipokuwa akimjibu shabiki kwenye mtandao wa Instagram, na kueleza kuwa umaarufu na namba za Zuchu zimeongezeka na ndiyo maana itahitajika kulipa kiasi kikubwa kama hicho ikiwa atakusudia kuondoka kwenye lebo hiyo.

Diamond aelezea sababu ya kuchukua 60% ya mapato ya wasanii WCB

Muimbaji huyo aliwahi kusema kwamba kampuni ya WCB inawekeza pesa nyingi kwa wasanii wanaowasaini na ndiyo maana wanavuma kwa muda mfupi.

“Tuko kwenye biashara ya muziki lakini mwanzoni kulikuwa na uvumi kwamba wasanii wananyonywa. Ilifika hata kwa Rais lakini tulijieleza tukisema hii ni biashara na waliielewa kwa mtazamo wetu,” amesema.

“Kwa hivyo huwezi kuondoka tu wakati tumewekeza mamilioni katika ufundi wako. Ninawekeza kwa watu hawa, nahakikisha wanapata jina, pamoja na shoo ili tupate pesa mwisho wa siku,” ameongeza.