Diamond alipwa TZS milioni 23 kwa dakika 1 katika mkutano wa Raila Odinga

0
57

Agosti 6 mwaka huu ilikuwa siku nzuri kwa msanii Diamond Platnumz kutoka Tanzania wakati mgombea Urais wa Kenya, Raila Odinga alipokuwa akijinadi katika mkutano wake wa mwisho kwa Wakenya kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanya Agosti 9 mwaka huu.

Msanii Diamond alijipatia mamilioni ya pesa katika mojawapo ya onesho fupi zaidi kuwahi kutokea maishani mwake, na kisha kurejea Afrika Kusini kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa binti yake,Tiffah.

Diamond aeleza sababu ya kuchukua 60% ya mapato ya wasanii WCB

Kwa mujibu wa tovuti ya Nation imebaini kuwa Diamond Platnumz alitumia takribani dakika 10 kutumbuiza onesho lake katika mkutano wa kumnadi Raila Odinga kisha kulipwa TZS milioni 233.1

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, Diamond Platnumz amekuwa akitoza TZS milioni 163.2 kwa onesho la saa moja nje ya Tanzania.

Send this to a friend