Diamond ashika namba 5 Afrika

0
71

Msanii Diamond Platnum ameshika nafasi ya tano barani Afrika kwa kuwa na wafuasi milioni 7.1 kwenye mtandao wa Youtube.

Pia anashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na wafuasi wengi zaidi Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Afrika Kusini.

Katika orodha hiyo, nafasi ya kwanza inashikwa na msanii Mohamed Ramadan kutoka nchini Misri akiwa na wafuasi milioni 14.2 na kufuatiwa na msanii Saad Lamjarred kutoka Morocco ambaye ana wafuasi milioni 14 Youtube.

Soolking msanii kutoka Algeria anashika nafasi ya tatu katika orodha hiyo akiwa na wafuasi milioni 9.5 huku namba nne ikishikwa na Tamer Hosny kutoka nchini Misri akiwa na wafuasi milioni 7.77.

Send this to a friend