Diamond: Ndio maana sishiriki Tuzo za BASATA

0
41

Mwanamuzki Diamond Platnumz ameonesha kukerwa na kitendo cha BASATA na TCRA kuufungia wimbo wa MTASUBIRI aliomshirikisha Zuchu, na kusema kwamba vitendo kama hivyo ndio vinasababisha asishiriki tuzo za nchini.

Barua ya wazi ya Zuchu kwenda BASATA na TCRA

Akiweka ujumbe katika ukurasa wa Zuchu, bosi huyo wa WCB amesema hajui sababu za wimbo huo kufungiwa kwa sababu maelezo yaliyotolewa na mamlaka hizo hayaoneshi hali halisi.

Katika ujumbe wake, Diamond amehoji, “Najiuliza kuna baya lolote limefanyika kwenye hio scene? Mlivaa vimini? hapana!… Nlitwerk ama Mliimba matusi humo kanisani? Hapana!.. Mlivuta sigara au bangi humo? Hapana!… Mlikiss ama Kunywa Pombe humo Hapana!… Simu iliita, ulipokelea ndani? Hapana…je kushoot kanisani ni sisi wa kwanza? hapana!”

TCRA yaufungia wimbo wa Diamond na Zuchu

Ameendela, “Kuna wengine walishoot Videos na Movie tena wao walifanya kwa kulidhalilisha kabisa kanisa… Nyimbo zao Zili fungiwa??? hapana! …. Halaf kesho utaniuliza kwanini Nilikataa kushiriki Tuzo za Basata…NCHI ya Wenyewe hii Zuuh… Kikubwa Mungu na Mashabiki wanatupenda hio inatosha…tuendelee kuwawakilishia Taifa lao, leo bendera inapeperukia Ethiopia InshaAllah :flag-tz:

Send this to a friend