Diamond Platnumz ashangaa mwili wake kuendelea kupungua

0
38

Kutokana na baadhi ya mashabiki na Watanzania kwa ujumla kushangazwa na mwoneko wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnum, kwa mara ya kwanza amezungumzia kuhusu mwonekano wa mwili wake akisema kuwa hata yeye haelewi sababu za kupungua.

Diamond Platnumz ameyasema hayo katika mtandao wa Instagram huku akionesha kushangazwa kutokana na kuendelea kupungua mwili wake kadiri siku zinavyokwenda.

Harmonize: Sijamdai Anjella hata senti moja

Alieleza kuwa si yeye pekee anayeshangazwa na mwili wake kuendelea kupungua bali hata Watanzania wote wamekuwa wakiibua maswali mengi kwenye mitandao ya kijamii.

“Halafu nimekuwa mdogo kila siku nazidi kuwa mdogomdogo. Hilo suala linawachanganya Watanzania wengi,” aliandika Diamond Platnumz.

Send this to a friend