Diamond Platnumz, mwanamuziki wa kwanza Kusini mwa Afrika kufikisha views bilioni 1

0
90

Mwanamuziki Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz ameweka rekodi nyingine kwa kuwa mwanamuziki wa kwanza Kusini mwa Jangwa la Saraha kufikisha views bilioni moja katika mtandao wa YouTube.

Kenya ilivyomfanya Diamond kuwa milionea

Diamond amefanya sherehe ndogo kusherehekea hatua hiyo kubwa katika muziki wa Tanzania na Afrika, ambapo hadi saa 10 jioni leo Juni 10, 2020, video zake zote zilikuwa na views 1,000,391,358.

Corona: Diamond Platnumz apata hasara ya TZS 3.5 bilioni

Chibu Dangote ukipenda muite Simba ana jumla ya wafuasi milioni 3.6 kwenye anuani yake ya YouTube ana amepakia (upload) jumla ya video 655.

Mbali na video za muziki, nyota huyo wa Afrobeat pia huweka video za nyuma ya pazia, matamasha yake ya muziki ndani na nje ya nchi.

Wasanii 5 wa Tanzania waliotazamwa zaidi kwa mwaka mmoja uliopita

Corona: Picha za hoteli ya Diamond Platnumz aliyotoa iwe karantini

Hivi karibuni Diamond alipata utambuzi mwingine ambapo Billboard ilimtolea Diamond kama mfano kwa wasanii wengine wanaotaka kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube.

Send this to a friend